Profesa Joyce Ndalichako ameagiza jeshi la polisi kuharakisha uchunguzi kifo cha mwanafunzi,
Waziri wa elimu, sayansi, teknolojia na
ufundi, profesa joyce ndalichako ameagiza jeshi la polisi kuharakisha uchunguzi
juu ya kifo cha mwanafunzi, akwilina akwilin aliyepigwa risasi na kufa, akiwa
kwenye basi katika eneo la kinondoni jijini dar es salaam.
Profesa ndalichako ameyasema hayo jijini dar
es salaam jana katika chuo cha taifa cha usafirishaji alikokuwa akisoma
mwanafunzi huyo.
Hapojana maelfu ya watu walimuagamwanafunzi
huyo , kabla ya kusafirishwa kuelekea kwao, rombo mkoani kilimanjaro kwa
mazishi, yanayotarajiwa kufanyika leo.
Profesa ndalichako amesema rais john magufuli
na viongozi wengine, wameguswa na msiba huo kufuatia kifo chake februari 16
mwaka huu, na ndiyo maana serikali iliamua kubeba gharama zote za msiba huo.
Ndalichako amesema serikali inachukua kwa
uzito mkubwa suala hili, na rais magufuli ameagiza vyombo vya ulinzi vifuatilie
pamoja na kutoa mwito kwa jeshi la polisi liharakishe uchunguzi huu ili haki
ipatikane kwani uchunguzi huo, pia utasaidia vitendo vya namna hiyo visiendelee
kutokea siku zijazo.
No comments