TUMBATU FM

Breaking News

IGP Sirro atoa onyo kwa wanaotumia Mitandao vibaya



MKUU wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, amewaonya baadhi ya watu wanaohamasishana kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu kufanya maandamano bila kufuata utaratibu uliopo na kwamba kitendo hicho ni kinyume cha sheria za nchi.

IGP Sirro amesema hayo akiwa Bariadi Mkoani Simiyu wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi ambapo ameonya harakati zenye kuhatarisha amani ya nchi huku akitoa wito kwa wazazi kuendelea kujenga malezi bora kwa watoto wao.

Hata hivyo IGP Sirro amewataka askari wa Jeshi hilo kote nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa kufuata misingi ya sheria na taratibu za nchi ikiwa pamoja na kuhakikisha wanatenda haki kwa wananchi wanaowahudumia na kutokujihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na kudhibiti matishio ya aina yeyote yatakayojitokeza.

No comments