Simba ya pania kurudisha heshima
Klabu ambayo imeanzishwa na mtu binafsi
ruksa unaweza kuipumzisha mwaka mzima wawe wanakuimbia nyumbani kwako, sawa.
Jasho la wananchi tumeliwekea masharti na sisi hatuko peke yetu duniani,
tumeiga mifano halisia katika nchi mbalimbali
Simba inataka kufanya kweli kwenye michuano ya Afrika baada ya
kushindwa kuliwakilisha taifa kwa misimu minne mfululizo, baada ya ratiba
kutolewa na shirikisho la soka Afrika, afisa habari wa Simba Haji Manara
amesema, wanataka kuendeleza rekodi yao katika michuano hiyo kwa sababu kwa
kipindi chote ambacho hawajashiriki mashindano ya kimataifa nchi haikuwa na
uwakilishi mzuri.
Manara amesema hakuna timu ya kubeza katika soka la sasa hususan
timu ambayo imepata uwakilishi katika mashindano ya vilabu Afrika.
“Ratiba tumeipokea na tumeona ratiba ambayo ipo sawa, wengi
wanaona kwamba Djibouti ni dhaifu lakini hivyo wanadhani ni ratiba nyepesi
kwetu lakini unapozungumzia mpira sasa hivi hakuna timu dhaifu, Djibouti
unaweza ukaona ni dhaifu kwa kuangalia FIFA ranking lakini timu ambayo imepata
uwakilishi kwenye CAF Confederation hatuwezi kuidharau hata kidogo.”
“Tutaipa umuhimu hiyo mechi na hatuta
wadharau na tunaona kama tunaenda kucheza na timu kubwa kwa sababu sisi malengo
yetu sio raundi ya kwanza, kwa sasa tunawaangalia Djibouti baada ya hapo Mungu
akijalia tukashinda tunaangalia timu inayokuja. Lengo letu ni kufanya vizuri
kwa sababu tumepigana kuipata nafasi kwa miaka minne na unajua nchi haikupata
uwakilishi mzuri kwa kipindi chote hicho kwa hiyo tunadhani tutaenda kuendeleza
rekodi yetu nzuri ya uwakilishi bora kwenye mashindano ya vilabu Afrika.”
“Sasa hivi tunaweka sawa masuala ya
kiusajili nadhani tarehe 15 au 16 nitawaita waandishi wa habari kuelezea
mipango na mikakati yetu kwa ujumla kuelekea January mpaka mwisho wa msimu huu
pamoja na mashindano ya kimataifa.”
No comments