Msanii wa injili ‘Bahati’ apania kuweka rekodi ya Cassper Nyovest nchini Kenya
Msanii wa muziki wa injili nchini Kenya, Bahati amepania kuweka rekodi ya kujaza watu katika uwanja wa mpira wa Thika kwenye tamasha lake kubwa mwishoni mwa mwaka huu.
Bahati anatarajia kutumbuiza mashabiki wake kwenye uwanja huo wa mpira ambao unaingia watu 5,000 katika tamasha aliloliita EMBJesusParty ambapo alianza kutangaza nia hiyo tangu mwezi uliopita mitandaoni kwa kutumia hashtag ya #TujazeThikaStadium.
Endapo atajaza huenda ikawa ni historia kwa Kenya kwa msanii mmoja wa injili kufanya hivyo kwani kwa idadi ya watu 5,000 sio kubwa sana kutokana na ukubwa wa jina lake nchini humo.
Wazo lake la kujaza limekuja baada ya kushuhudia rapper mkubwa nchini Afrika Kusini, Cassper Nyovest kuvunja rekodi zake yeye mwenyewe kwa miaka mitatu mfululizo.
Bahati ni moja ya wasanii wakubwa wa muziki wa injili Afrika ambao walimpongeza Cassper Nyovest kwa kujaza uwanja wa mpira jumamosi iliyopita kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika “The African Music Industry ;We Are All Proud of this Big Brother @casspernyovest for Making History Filling Up 5th Largest stadium in the World!!! And Am here Praying/ Asking God/Telling/ Believing God that History haitakua ina Makiwa na South African’s & West Pekeee- I believe in Kenyan Fans & Musicians #KENYAITSOURTURN Let’s Start Somewhere This 31st December All Roads head to #THIKASTADIUM”
Tamasha hilo la EMBJesusParty litafanyika tarehe 31 Desemba 2017. Na kiingilio cha show hiyo ni shilingi 200/= za Kenya ambayo ni sawa na Tsh 4,500.
No comments