TUMBATU FM

Breaking News

Kocha wa Man United Mbion kumsajili Gareth Bale.



Kocha  wa Manchester United, Jose Mourinho anaamini straika wake Zlatan Ibrahimovic aliyerejea uwanjani hataweza kucheza vizuri kama ilivyo-kuwa awali, hivyo yupo mbioni kumsajili Gareth Bale.

Kwa muda mrefu Mourinho amekuwa akihusishwa na mipango ya kumuhitaji Bale kutoka Real Madrid ili akaongeze nguvu ya ushambuliaji katika kikosi chake.

Habari kutoka Man United, zimeeleza kuwa Mourinho anataka kumfanya Bale kuwa usajili muhimu katika usajili ujao wa Januari ili kuimarisha kikosi chake katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ligi Kuu England.

Awali, ilionekana kama ni vigumu kwa Bale raia wa Wales kutua Man United lakini sasa inaonekana Madrid inaelekea kuchoka kuwa na mshambuliaji huyo ambaye ana majeraha ya mara kwa mara.

Licha ya kuonekana kuwa na nia ya kumuuza, Madrid imeweka dau la pauni milioni 79 kwa Bale japokuwa awali Man United inadaiwa kuweka mkakati wa kutolipa zaidi ya pauni milioni 65 ili kumsajili Bale.

Tottenham Hotspur inaonekana kutaka kuizidi kete Man United, lakini mazungumzo ya mwanzoni mwa msimu huu kati ya Bale na Man United yanampa nafasi Mourinho ya kumnasa mchezaji huyo.

Mourinho anaelezwa kuweka presha ya kumsajili Bale kwa kiasi ambacho Madrid watakitaka huku akibaki na mbadala wa Antonie Griezmann wa Atletico Madrid endapo ishu ya Bale ikibuma.

Jumatano wiki hii, Bale aliifungia Madrid bao moja katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Al Jazira katika nusu fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia huko Falme za Kiarabu.

Madrid imepanga ikimuuza Bale iwasajili mmoja au wote kati ya Aubameyang, Dybala na Eden Hazard.MANCHESTER, England

No comments