TUMBATU FM

Breaking News

Baada ya vyuma kukaza, Jike Shupa aamua kuwa mpishi



Zena Abdallah ‘Jike Shupa’.

MUUZA sura kwenye video mbalimbali za wasanii wa Bongo Fleva, Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ ameamua kugeukia mapishi baada ya kuona vyuma vimekaza ambapo anapika vyakula kwenye shughuli mbalimbali ili kujikwamua kimaisha.

Akipiga stori na Risasi Jumamosi, Jike Shupa alisema kila kukicha maisha yanazidi kuwa magumu ambapo kwa sasa ameamua kuachana na kuendekeza starehe na kuishi na mashoga ‘wanaume tata’ nyumbani kwake na kugeukia mapishi ambapo anapika vyakula vya tenda kwenye shughuli mbalimbali.

“Yaani nimeona nitakufa njaa ndiyo nikaamua kuwafukuza mashoga wote na kuanza kufanya kazi hii ya kupika kwenye shughuli hivyo nachukua tenda napika na watu wangu, naona inanilipa na ni afadhali maana nilikuwa naendekeza starehe za kulala tu ndani na kutegemea wanaume lakini sasa hivi nafanya kazi napata fedha kwa nguvu zangu,” alisema Jike Shupa.

No comments