Chama cha mapinduzi kimetangaza majina ya wagombea wao
Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imepitisha majina matatu
ya wagombea ubunge watakaopeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi
mdogo utakaofanyika Januari 13, mwakani.
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama
hicho Humphrey Polepole leo Desemba 15, imewataja waliopitishwa kuwa ni Monko
Justine Joseph (Singida Kaskazini), Damas Ndumbaro (Songea Mjini) na Dk Stephen
Lemomob Kiruswa (Longido).
Amesema CCM kinawatakia wagombea hao maandalizi mema ya uchaguzi
chini ya uongozi wa uratibu wa mkoa, wilaya na majimbo husika.
“ Hii itajumuisha kuchukua fomu za uteuzi kutoka Tume ya Taifa
ya uchaguzi (NEC) kuanzia Kesho Disemba 16,” amesema.
Wakati CCM kikitangaza wagombea wake, Chama cha ACT-Wazalendo
kinakutana kesho jijini Dar es Salaam kujadili uchaguzi huo huku Chama cha
Wananchi (CUF) tayari kikiwa kimepitisha wagombea wake.
Cc: Mwananchi
No comments