MAJALIWA AKEMEA DHARAU TRA
Majaliwa ametoa leo Jumatatu Mei 15, 2023 alipokuwa akizungumza na wafanyabishara wa Kariakoo kufuatia mgomo walioutisha kutokana na kero mbalimbali wanazodai zinatokana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Baadhi ya kero walizotaja wafanyabiashara hao ni kamata kamata ya TRA dhidi ya wafanyabiashara na wateja kutoka nchi jirani wanaofanya manunuzi katika soko hilo na ulazima wa kusajili maghala yanayohifadhi bidhaa kitu ambacho kimekuwa kero na kukosa majibu kwa viongozi waliofika sokoni hapo.
Kutokana na hatua hiyo, Majaliwa amesema: “Hakuna mtumishi wa Serikali anayepaswa kumdharua kiongozi wake wa juu, Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.
Majaliwa amesema Rais anapotoa agizo wao kama wasaidizi wake wanapaswa kulitekeleza. Amesema Rais Samia aliagiza madai kodi ya miaka mitano nyuma kwa wafanyabiashara, wasidaiwe; lakini TRA wanawaambia watoe barua kuhusu suala hilo.
Amesema Serikali ina taarifa za uwepo wa kikosi kazi kilichoundwa kuzunguka eneo la Kariakoo akisisitiza pamoja na kazi nzuri inayofanywa na mamlaka hiyo katika kukusanya kodi, Rais Samia amekemea vikosi kazi vyenye kuwa kero kwa wananchi.
No comments