TUMBATU FM

Breaking News

Siko tayari kuiacha Simba - Asante Kwasi

Image result for asante kwasi

Beki wa Simba SC, Asante Kwasi ameonyesha hali ya kuigomea klabu hiyo akisisitiza hayupo tayari kuondoka kizembe Msimbazi, hata kama watahitaji kumtoa kwa mkopo.

Kwasi alijiunga na Simba kwenye dirisha dogo la usajili msimu uliopita akitokea Lipuli FC ya Iringa, kwa mkataba wa miaka miwili ambapo mkataba wake unatarajiwa kumalizika Desemba, mwaka huu, huku mchango wake ndani ya klabu hiyo ukiendelea kuwa mdogo zaidi.

Kwasi alisema, pamoja na mkataba wake wa kuitumikia Simba kubakiza miezi mitano tu, hatakubali kuiacha kizembe hata kama viongozi wake watataka kumtoa kwa mkopo.

“Napenda sana kuendelea kuitumikia Simba kwa msimu ujao, pamoja na kuwa na muda mfupi wa kucheza kwa sasa.

"Siko tayari kuiacha Simba, ila nitajitahidi kupambana kadiri ninapopewa nafasi za kucheza na kocha ili nionyeshe mchango hasa kwa msimu ujao kwani msimu huu umekuwa mgumu kwangu baada ya kukabiliwa na majeraha ya mara kwa mara.

No comments