Watumishi wa afya waaswa kujiepusha na vitendo vya rushwa
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjuCxTOLbvElEX4cO4cELgDWNY7ojuys7KSPeARmkzcWT1l1DGgKcIh-e_POxjeLp-FRc7ojgvOPF0urors0DRtvYhG68ALK9JVgHxdesQk5cOqtNffWAxyrz64bjpwWRq9m4aWLvSK8Dk/s640/MWALIMUUMMY.jpg)
WATUMISHI wa sekta ya Afya nchini wametakiwa kujiepusha na vitendo vya kutaka rushwa kutoka kwa wananchi wanapokuwa sehemu zao za kazi ili kuendana na maadili ya utumishi wa Umma.
Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kilichofanyika leo jijini Dar es salaam ili kujadili mustakabari wa utoaji huduma za Afya nchini.
“Marufuku Watumishi wa sekta ya afya nchini kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa na kama wapo naomba waache mara moja kwani atakayebainika anajihusisha na rushwa sheria itafuata mkondo wake mara moja” alisema Waziri Ummy. Aidha Waziri Ummy amesema kuwa watumishi wa sekta ya afya hasa katika sehemu ya kutolea huduma za afya wanatakiwa kuwa na lugha nzuri kwa wananchi pindi wanapotoa huduma sehemu zao za kazi.
No comments