TUMBATU FM

Breaking News

Wahamiaji haramu 14 wafarik



Watu 14 wamefariki na wengine 6 hawajulikani walipo baada ya mtumbwi waliokuwa wakitumia kusafiri kuelekea katika kisiwa cha Agothinisi ambacho ni milki ya Ugiriki kuzama .
Mtumbwi huo ulikwa ukiwasafirisha watu 20 wakiwemo watoto na wanawake.

Kikosi cha wanamaji cha Ugiriki cha shirika la FRONTEX kiliwaokoa  watu wengine walikuwa wakitaka kuzama  wakielekea nchini Ugiriki.

Hata hivyo shughuli za uokozi zinaendelea katika bahari ya Egean na kuimarisha ulinzi kwa kuwa safari kinyume na sheria kuelekea nchini Ugiriki zimeongezeka kutokana na msimu wa baridi umeanza kumalizika

No comments