TUMBATU FM

Breaking News

Urusi yawatimua wanadiplomasia 23 wa Uingereza



Urusi imewataka wanadiplomasia 23 wa Uingereza kuondoka ndani ya wiki moja.

Uamuzi huo umetangazwa na wizara ya  mambo ya nje ya Urusi baada ya kufanya mazungumzo na balozi wa Uingereza nchini humo Laurie Bristow.

Baada ya Uingereza kuamua kuwafukuza wanadiplomasia 23wa Urusi,Moscow imeamua pia kufunga baraza la Uingereza nchini Urusi na vilevile kuondoa ruhusa ya Uingereza kufungua ubalozi mkuu mjini St.Petersburg.

No comments