Tumbatu, Uongozi wa CCM unapokea mawazo kwa wanachama wao
uongozi wa jumuiya ya vijana wa chama cha mapinduzi ccm jimbo la
tumbatu umesema unaendelea kusikiliza mawazo na ushuri kutoka kwa wanachama na
viongozi wengine ili kupata mawazo yenye tija ambayo yatapelekea kukikuza
chama.
wakizungumza na radio jamii tumbatu mara baada ya kumaliza kikao
maalum kilichowahusisha viongozi wa jumuiya hio mwenyekitiwa jumuiya ya vijana
jimbo la tumbatu abdurazak mwadini
makame na katibu wa jumuiya haji
sharifu haji wamesema wameamua kufanya hivyo ili kuwashirikisha wanachama wao
katika kila hatua inayopitiwa na jumuiya
katika kukuza maendeleo ya chama.
viongozi hao wamesema watajitahidi kuyafanyia kazi mawazo ya wanachama
wao ya kuibua miradi ya jumuiya ili kuachana na utegemezi wa viongozi na hivyo
kudumaza maendeleo ya chama
kwa upande wake mmoja wa washiriki wa kikao hicho ali moh'd ussi
amesema mpango wa kuwahusisha wanachama na
viongozi katika kuibua mawazo ni kuwataka viongozi kuwa makini katika kuchanganua
mawazo ya kila mtu ili mawazo hayo yaweze kutumika kwa wakati muafaka na sio
kuchagua na kuaacha ya baadhi ya watu kitendo ambacho kinaweza kukatisha tamaa
na kutoa matumaini kwa watoaji wa mawazo hayo.
kikao cha jumuiya ya vijana ya chama cha mapindizi jimbo la tumbatu
hufanyika kila mwaka kwa lengo la kutathimini maendeleo ya jumuiya katika
kukuza maendeleo ya chama.
No comments