TUMBATU FM

Breaking News

Rais Emmerson avutia wawekezaji



Rais Emmerson Mnangagwa amewataka wawekezaji nchini Zimbabwe wasiwe na wasiwasi kuhusu hali isiyotabirika ya kisiasa kutokana na uchaguzi mkuu utakaofanyika katikati ya mwaka huu.

Rais Mnangagwa amesema Zimbabwe ni nchi ya amani, na anakaribisha nchi zote kufanya biashara na nchi yake katika mazingira ya amani.

Ameongeza kuwa serikali ya Zimbabwe itahakikisha uchaguzi mkuu unafanyika kwa uhuru, haki na kuaminika, kwa kulingana na kanuni za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC na Umoja wa Afrika.

Amesema serikali ya Zimbabwe inajiandaa kuhimiza mageuzi ya kiuchumi, ili kuongeza uwezo wa ushindani wa nchi hiyo, na kuifanya Zimbabwe iwe nchi inayovutia zaidi uwekezaji barani Afrika.

No comments