TUMBATU FM

Breaking News

Okwi, Bocco, waombewa ulinzi

Image result for Okwi images
Ligi kuu Tanzania bara inatarajia kuendelea tena Ijumaa ya Machi 3, 2018 kwa mechi moja kati ya Simba dhidi ya Stand United mchezo utakaochezwa uwanja wa taifa kuanzia saa 10 jioni.
Haji Manara amewaomba waamuzi wa ligi kuu kuwalinda wachezaji ma-star ili kuwaepusha na majera yasiyo ya lazima hususan katika kipindi hiki ambacho baadhi ya timu zinawakilisha nchi katika mechi za mashindano ya Afrika.
“Hakuna wachezaji wapya wenye majeraha zaidi ya Okwi na John Bocco ambao kwa kiasi fulani wametengemaa na kama mwalimu itampendeza akiamua kuwatumia basi wanaweza wakawepo uwanjani.”
“Walipata majera na katika hili lazima tuwaombe bodi ya ligi na waamuzi, hatutaki wachezaji wetu wawe special lakini kwenye mpira kokote duniani si vyema nyota wakawa wanakosekana uwanjani katika michezo tofautitofauti kwa sababu ya majeruhi ambayo yanasababishwa na rafu ambazo hazistahili kuchezwa kwenye mpira.”
“Tunaomba waamuzi waendelee kuchezesha kwa haki kama wanavyofanya lakini FIFA wana kauli yao ya kulinda wachezaji nyota wanasema ‘wachezaji nyota hulindwa’ kwa sababu watu wanakwenda viwanjani sio kuangalia tu timu, wanaangalia na wachezaji nyota kama Okwi, Chirwa, Samatta, Ronaldo, Beckham.”
“Kwa hiyo lazima ifike mahali waamuzi wajue baadhi ya mabeki wanaweza kufanya rafu ambazo zinaweza kutugharimu kwa sababu Simba tunawakisha nchi na baada ya mechi ya Stand Jumatano tutacheza na Al Masry.
John Bocco aliumia kifundo cha mguu wa kusho kwenye mchezo wa ligi kati ya Mwadui dhidi ya Simba uliochezwa uwanja wa Kambarage, Shinyanga lakini Emanuel Okwi yeye alipata majeraha wakati wa mchezo wa ligi kati ya Simba dhidi ya Mbao uliochezwa uwanja wa taifa.

No comments