TUMBATU FM

Breaking News

Ndege za kijeshi za Israeli zashambulia kundi la Hamas eneo la Gaza

Image result for Israil images

Ndege za kijeshi za Israeli zimeshambulia vituo vya Hamas usiku wa kuamkia Jumapili katika ukanda wa Gaza, baada ya kutokea mlipuko karibu na uzio kati ya Israeli na Palestina.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa jeshi, ndege hizo zililenga kituo kilichopo katikati ya Gaza kinachomilikiwa na kundi la kiislamu la Palestina la Hamas linalodhibiti ukanda wa Gaza.

Taarifa hiyo imesema, mlipuko uliotokea jana, haukusababisha majeruhi, kwa vile vikosi vya askari havikuwepo jirani na eneo hilo.

Hadi sasa hakuna kikundi kinachoshukiwa kuhusika na shambulio hilo, lakini jeshi linalihusisha kundi la Hamas kwa mashambulizi yote ya ukanda wa Gaza.

Wakati huo huo, jeshi la Israeli linamshikilia raia wa Palestina anayetuhumiwa kuhusika na shambulio la kuchoma kisu lililotokea mwezi februari. Habari zinaeleza kuwa, raia huyo wa Palestina alikamatwa Jumapili katika mji wa ukingo wa Nablus wakati wa msako uliofanywa na Wanajeshi na askari katika eneo la Shin Bet.

No comments