TUMBATU FM

Breaking News

Msuva asema amejifunza mengi Difaa El Jadidda



Winga wa kimataifa wa Tanzania Simon Msuva anayekipiga kwenye klabu ya Difaa El Jadidda amesema amejifunza mengi ndio mana watu wanasema nimebadilika kiuchezaji.

''Kuna kitu flani watu wanasema Simon amebadilika na ni kweli kwasababu hata mimi nilivyokuja kcuheza timu ya taifa niliona kabisa uwezo umeongezeka hivyo ni kweli nimejifunza vitu vingi kwa kucheza nje'', amesema.

Kwa upande mwingine Msuva amemshukuru kocha wa Taifa Stars Salum Mayanga kwa kumujumuisha kwenye kikosi kitakachocheza mechi za kimataifa za Kalenda ya FIFA dhidi ya Algeria na DR Congo.

Aidha Msuva ameongeza kuwa ataendelea kujituma zaidi na kufuata maelekezo ya waalimu wake ili azidi kufika mbali zaidi kwani bado hajafika sehemu ambayo anaona inatosha.

No comments