TUMBATU FM

Breaking News

Waziri Mkuu awapa ujumbu huu kina Dkt. Slaa



Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa amewataka mabalozi watumie mbinu za kidiplomasia kuvutia wawekezaji katika sekta mbalimbali, ikiwemo ya utalii na kutafuta masoko ya bidhaa zinazozalishwa nchini

Kassim Majaliwa ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na Balozi Dkt. Wilbrod Slaa anayewakilisha Tanzania nchini Sweden, na Balozi Muhidin Ally Mboweto anayewakilisha Tazania nchini Nigeria, katika makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam , na kuwataka mabalozi hayo wakaimarishe diplomasia waendako

Waziri Mkuu amesema Tanzania ina vivutio vingi vya utalii  hivyo ni vema wakajielekeza katika kuvutia wawawekezaji kwenye sekta hiyo ili Taifa lipate watalii wengi, na wawekezaji kwa ajili ya kuwekeza kwenye sekta ya madini, viwanda na kutafuta masoko ili wafanyabiashara na wakulima wa Tanzania waweze kuuza bidhaa zao nje ya nchi.

“Tumejiimarisha katika mazao ya chakula na biashara, hivyo tunatakiwa kuwa na uhakika wa masoko kwenye kilimo ili mkulima anapozalisha pamba, tumbaku, kahawa, chai, korosho, dengu pamoja na mazao mengine tuwe na mahali pa kuuza, kwa hiyo washawishini wafanyabiashara kuja kununua", amesema Kassim Majaliwa.

Pia Waziri Mkuu amewataka mabalozi hao wakawatambue na kuwaunganisha Watanzania waishio kwenye nchi wanazoiwakilisha,  ili nao washiriki kwenye ujenzi wa uchumi wa viwanda na kuwasisitiza wakumbuke nyumbani.

No comments