TUMBATU FM

Breaking News

Wachezaji wawili wa Azam FC warejea Uwanjani



Wachezaji wawili wa klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Nahodha Himid Mao na mshambuliaji Wazir Junior wamerejea rasmi uwanjani kwa kuanza kufanya mazoezo mepesi mepesi baada ya kukosekana kwa kipindi kirefu kutokana na kuwa majeruhi.

Himid alikuwa akisumbuliwa na maumivu chini ya goti la mguu wake wa kulia huku Junior akikabiliana na tatizo katika kifundo chake cha mguu wa kulia na kusababisha kusababisha wapenzi wa timu hiyo kushindwa kupata radha zao wakiwa wanalisakata kabumbu.

Aidha, Waziri Junior amesema anamshukuru Mungu kwa kuweza kurudi tena katika kikosi na kuahidi kujituma kama alivyokuwa awali.

"Kutokana na majeruhi haya ndio ilikuwa hivyo lakini tutapambana kama ilivyokuwa mwanzo, nimeu-miss sana mpira, kucheza na hata kuonyesha vile mashabiki wanataka. Lakini naamini kwa rehema za mwenyezi Mungu tutakaporejea tena basi mashabiki watafurahia vile walivyokuwa wakivisubiria", amesema Junior.

Ujio wa nyota hao umekuja wakati kikosi chao kikijiandaa na michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida United mchezo unaotarajiwa kupigwa katika dimba lao la nyumbani Azam Complex nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam siku ya Jumamosi.

No comments