TUMBATU FM

Breaking News

Serikali kupitia idara watu wenye ulemavu imeweza kutoa mafunzo ya lugha

Image result for Serikali ya mapinduzi zanzibar

Serikali   ya  mapinduzi  ya  zanzibar  kupitia  idara  ya  watu  wenye  ulemavu  imeweza  kutoa  mafunzo  ya  lugha  za  alama  kwa  wafanya  kazi  wa  taasisi mbalimbali   ikiwemo polisi, wafanya  biashara    na  madereva.

Akifungua   kongamana  la  kuhamasisha  lugha  za  alama  zanzibar   spika  baraza  la wawakilishi  zanzibar  zubeir  ali  maulid   .amesema  kuwa  mafunzo  hayo  yana  lengo  la  kuwafanya  watu  mbalimbali  kuilewa  na  kuitumia  lugha  hiyo  pale  wanapokutakana  na  watu  wenye  ulemavu  ndani  ya  maofisi  yao  au  ndani  ya  jamii.

Kwa   upande  wao  walimu  wa  lugha  za  alama  wamesema  kuwa  changamoto  kubwa  kwao  ni  kutokuwepo  kwa  wakalamani  katika  vyombo   vya  habari hali  na kwakosesha haki yao ya msingi ya kupata habari  kwa watu wenye ulemavu.

katika   kongamano  hilo   mada  tatu   zimewasilishwa ikiwemo  haki  na  fursa  kwa  watu  wenye  ulemavu  ,umuhimu  wa  lugha  za alama  na  dhana  jumuisho.


No comments