Rage: Simba ina nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa iwapo haitabweteka
MWENYEKITI wa zamani wa Simba, Ismail Aden Rage, amesema kuwa hakuna kitu kitakachoizuia timu hiyo kutangaza ubingwa mapema msimu huu.
Simba inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 42, huku Yanga wakiwa na pointi 37, wakiwa wametofautiana pointi tano tu lakini Rage amesisitiza kuwa kama Simba hawatabweteka, mapema tu watatangaza ubingwa.
“Simba ina nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa iwapo haitabweteka, timu nyingi kwa sasa zina udhamini wa kutosha, hivyo kusababisha ushindani kuwa mkubwa kwenye ligi, hivyo hawapaswi kuridhika na matokeo.
“Wachezaji wanatakiwa watambue kwa sasa wana jukumu moja tu la kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu, timu ambayo ilikuwa inatishia kidogo ilikuwa Azam lakini kwa sasa yenyewe haipo vizuri sana, hivyo bado inayo nafasi ya kufanya vizuri.
“Ushindani jinsi ulivyo hakuna aliyetegemea Mbao ingetolewa na Njombe Mji kwenye FA, wachezaji wa Simba wasibweteke hata kidogo, waonyeshe nguvu ya kuweza kufanya vyema kwenye ligi,” alisema Rage.
No comments