TUMBATU FM

Breaking News

Mwanamke anusurika kuuwawa na Papa



Mwanamke mmoja nchini  Australia mwenye umri wa miaka 55 amenusurika kifo jioni ya jana February 23, 2018 baada ya kushambuliwa na papa wakati anaogelea baharini katika eneo la Sydney Kusini-Mashariki.

Inaaminika kuwa papa huyo alikuwa na urefu wa kati ya mita 2.7 hadi 3.2. Mwanamke huyo alikimbizwa hospitali ya St George kupatiwa matibabu ambapo alikuwa amejeruhiwa kwenye mguu wake wa kulia.

Wakazi mbalimbali wa eneo hilo waliliambia shirika la utangazaji nchini Australia la ABC kuwa tukio hilo limewashtua kwani halijatokea kipindi cha zaidi ya miaka 25 hivyo ni la ajabu.

Mwanamke huyo amefanyiwa upasuaji na afya yake imeanza kuimarika.

No comments