Matokeo ya Urais Shule ya Secondary Tumbatu gomani
Tume ya uchaguzi shule ya secondary Tumbatu
gomani imemtangaza ndg kombo mwadini Khamis kuwa Rais wa shule hiyo kwa kupata
74 % ya kura na kumzidi mshindani wake Ndg Juma omar kwa kupata 24 % ya kura zote zilizopigwa.
Akitangaza matokeo hayo mwenyekiti wa Tume hiyo
Ndg Juma Makame khamis amesema Ndg Kombo mwadini amepata kura 510 sawa na 74%
na mshindani wake kupata kura 158 sawa na 24%
kati ya kura 669 halali
zilizopigwa na kura 5 kuharibika huku ikiwa idadi ya wanafunzi wote
walioandikishwa kupiga kura ni 749 na ambao hawa kujitokeza kupiga kura ni wanafanzi 76, ambapo
mwenyekiti huyo alishindwa kutaja sababu
iliyopelekea baadhi ya wanafunzi
kushindwa kujitokeza kupiga kura hapo
jana.
Amesema kuwa uchaguzi umeenda vizuri na ulikuwa
wa huru na haki huku akisema kuwa
hakuna mgombea yoyote aliejitokeza kutoa
malalamiko kuhus mchakato wa uchaguzi huo wa kumchagua rais shuleni hapo.
Akitoa neno la shukurani baada ya kutangazwa kuwa
Rais wa Wanafunz shuleni hapo Ndg kombo
Mwadini amesema kuwa kipaumbele chake
ni kuboresha elimu na kujenga heshima kwa wanafunzi wote shuleni kwa kuwashajihisha wanafunzi kupenda kusoma
na kuaacha mambo ambayo yanaweza kuwa felisha kwenye masomo yao, huku akiahidi
kuw hatowavumilia wanafunzi ambao watafanya utovu wa nidhamu huku wakitarajia
kupata mwavuli wake kama Rais shulen hapo huku akiwaomba walimu na wanafunzi
kutoa mashirikiano yao kwani bila ya wao yeye hatoweza kuiongoza shule hiyo.
Nae mwalimu Khadija Mohd Uss ambae ni mwalimu wa
ushauri nasaha shuleni hapo amesem kuwa wanawake wamekuwa nyuma kwenye mambo ya
kinyanganyiro cha uongozi huku akiwataka wanawake kujitokeza kugombea nafasi
hizo pale zinapojitokeza ili kujenga kujiamini kupata uzoefu kwenya maisha ya baadae.
Akihitimisha zoezi hilo mwalim Mdhanimi wa
serikal ya wanafunzi mwalimu juma gora amewataka wanafunzi kutekeleza sheria
zitakazosimamiwa na serikal mpya ili kuharakisha uapatikanaji wa maendeleo.
No comments